Bethel Radio

About

Bethel (Web) Radio ni redio ya kikristo yenye mtazamo wa kisasa inayotangaza kupitia mtandao wa Internet masaa 24, kwa lugha ya kiswahili. Redio hii inarusha matangazo yake kutoka Jijini Dar es salaam, Nchini Tanzania.

Radio hii imejikita kutangaza habari njema za ufalme wa Mungu (Ambalo ni agizo kuu – Mathayo 28:19 ) na Injili thabiti ya Yesu Kristo kwa njia ya Muziki, Vipindi, Mahubiri na Matangazo ya moja kwa moja (Mubashara) ya Semina, Makongamano, Mikutano, Matamasha na Ibada. Bethel Radio endesha progamu zake kwa kushirikiana na Makanisa na Huduma mbali mbali zinazo mtangaza na kumuamini Yesu Kristo .

Kupitia mtandao mkubwa wa internet Bethel Radio inawafika zaidi ya wasikilizaji 10,000 kwa siku, Kutoka mataifa zaidi ya 200 Duniani. Huku idadi ya wasikilizaji wengi wakipatika eneo la Africa Mashariki.

Bethel Radio imefanyika Lango na Madhabahu ya Mungu kukutana na haja za watu na kuwapa tumaini jipya (Mwanzo 28:16-19)

 

Na uwe wa kwanza kupata habari